Type Here to Get Search Results !

Azam Fc yatambulisha kocha mpya kutoka Senegal

 


Klabu ya Azam FC imemtangaza kocha Youssouph Dabo raia wa Senegal kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao na amesaini mkataba wa miaka mitatu. Dabo ni kocha wa zamani wa klabu ya Tenguteh FC ya Senegal iliyofuzu makundi ya klabu bingwa Afrika msimu 2020/21 kwa kuitoa Raja Casablanca ya Morocco.
-Dabo baada ya kuachana na Tenguteh FC iliyokuwa na akina Pape Sakho aliyepo Simba na Malikcou Ndoye aliyepo Azam alijiunga na timu ya Jaraaf de Dakar ya Senegal na April 10, 2023 timu hiyo ilitangaza kuachana na Dabo kwa makubaliano ya pande mbili kutokana na matokeo mabaya.
-Ila baada ya kauli hiyo Dabo alitangaza kuwa alishaachana na timu hiyo tangu mwanzoni mwa mwezi February na sababu kubwa ikitajwa ni kauli yake aliyoitoa kwenye bodi ya timu hiyo kwa kuwaambia mwishoni mwa msimu huu ataondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na moja klabu nchini Tanzania


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad

Hollywood Movies