Type Here to Get Search Results !

NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-04 HADI 6



( 4-6 )
🔥📚

NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-04

Ilipoishia..
Ghafla,nilistuka usiku.Kiza kilitawala,upepo mkali wa baridi ulipuliza.Nikaangaza macho huku na kule bila kuona chochote.Ghafla macho yangu yakafunguliwa mbele yangu nikamuona jini Vumina.Tulikuwa ndani pori kubwa.Harufu kali ya marashi ilitawala.
Jini vumina akataka nimpatie jibu lake.

Endelea..

"Mhh! Nakusikiliza,nipe jibu langu,lakini naomba utambue tu kuwa yote ninayokuambia hayana utani kabisa.Utakalo amua ndiyo itakuwa kesho yako"
Aliniambia jini huyo mrembo kwa kumtazama lakini ndaniye ni kiumbe wa kutisha.
Ulipita ukimya wa muda nikiwa natafakari,kisha nikanyanyua uso wangu na kumtazama msichana huyo aliyekuwa amejisogeza karibu yangu na kunipa wasaa wa kuuona vyema uso wake uliopambwa na midomo iliyotiwa nakshi kwa rangi ya bluu huku macho yake makubwa ya mviringo yakinitizama kwa haiba ya utulivu,harufu nzuri ya marashi yake ilipenya vilivyo katika pua zangu na kusababisha nijikute nikizidi kumtazama msichana huyo.
"Hivi kweli Vumina nikikubali kukuoa mke wangu atakuwa na nafasi gani?.Huoni kama hapo yanaweza kuibuka mengine"
"Usijali kwa hilo.Mimi nipo tayari kuwa na wewe kwa vyovyote vile,hata kama utaendelea kuwa naye.Ninachohitaji zaidi kutoka kwako ni ukubali kunioa nikiwa namaana ukubali kufunga ndoa na mimi"
Alinijibu jini Vumina huku akitabasamu na kuzidi kujenga hali ya tofauti kabisa ndani ya moyo wangu kwani nilijikuta ghafla nikianza kutamani kuwa naye.
"Basi usijali.Nimekubali kukuoa,lakini naomba  nafasi ya mke wangu ibaki kama ilivyo"
Nilimjibu jini huyo ambapo papo hapo ghafla mke wangu na mwanangu walionekana kitandani wakiwa wamelala fofofo.Kisha Vumina akanishika mkono na kuniambia alitaka tukatembelee kwao.
"Tunaenda wapi usiku huu Vumina,si bora tungeenda kesho wakati kuna mwanga"
"Wala hata usijali we nishike vizuri mkono wangu kisha funga macho"
Nilifanya kulingana na maagizo yake ambapo baada ya sekunde kadhaa jini Vumina akaniambia nifungue macho.Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni..huwezi amini nilipofungua macho yangu nilikuwa na Vumina katika sehemu nyingine kabisa iliyokuwa ikiangazwa na jua.Sehemu hiyo ilikuwa ya kuvutia kwelikweli.Kulipambwa kwa vijito vilivyokuwa vikitiririsha maji yaliyokuwa yakinyesha maua yaliyopendeza yaliyotoa harufu nzuri mno.Kwa sasa Vumina alikuwa ameavaa mavazi mengine tofauti na aliyokuwa amevaa wakati tukiwa kule chumbani kwangu.Alipendeza maradufu lakini nilipomtazama miguuni,niliingiwa na hofu kutokana na kuziona kwato zake zilizopambwa kwa manyoya meupe.
"Usiogope mume wangu,huna budi kunizoea maana utaishi na mimi mpaka kifo kitakapo tutenganisha"
Alisema Vumina maneno yaliyonikumbusha kipindi cha nyuma usiku wa ndoa yangu na mke wangu.
Tulishuka korongo dogo na kuingia katika sehemu iliyokuwa na kidimbwi ambacho kilijazwa kwa maji yaliyokuwa yakianguka kutoka kwenye maporomoko madogo.
Jini Vumina akaingia majini na kuzama kiasi,ikabaki sehemu ya mabega yake kupanda juu.
"Njoo ukae kwenye mabega yangu ndio tunakaribia kufika nyumbani"
Aliniambia Vumina.
Kwa woga nikamkalia mabegani lakini tofauti na matarajio yangu kwamba msichana huyo angeweweseka na kuzama,jini Vumia alianza kuzama dimbwini taratibu bila kutetereka mpaka uso wake ulipomezwa na maji kisha na mimi nikaanza kuzama.Maji yaliponifika shingoni nilianza kupiga kelele za yowe nikilitaja jina la jini huyo lakini wakati hayo yakiendelea ghafla tulijikuta katikati ya umati mkubwa wa watu.Tulikuwa wakavu kabisa bila kuwa na dalili yoyote ya kuzama majini.Cha kushangaza zaidi nilivaa mavazi mengine kabisa,yaliyoonekana ya gharama mno.Kanzu ndefu ya kiislamu iliyopambwa kwa mistari ya dhahabu pamoja na kitambaa kingine kilichoviringishwa kimtindo shingoni mwangu.Jini Vumia yeye ndiyo alikuwa aking'aa kama malikia.Mikononi alishika pete ambayo alitakiwa anivalishe.Umati ule mkubwa wa watu waliokuwa na asili ya Somali walianza kuimba nyimbo fulani iliyokuwa nzuri sana kusikiliza.Kisha kauli iliyosikika kutoka katika vipaza sauti ambavyo havikuonekana ilizungumza ikihitaji ukimya.Watu wote wakatulia.
Sauti hiyo ikaendelea.
"Vumia bin Zahur umekubali kwa moyo mmoja kumpokea binadamu huyu kama mumeo na unahakika atakuwa wa pekee maishani mwako?"
Sauti hiyo iliuliza swali kwa jini Vumia.
"Ndiyo nimekubali nikiamini kwa moyo mmoja"
"Je,wewe binadamu umeridhia kwa moyo mmoja kuishi na Vumia bin Zahur kama mkeo ukimfanya kuwa wapekee katika moyo wako?"
Swali hilo likawa kama limeirudisha akili yangu katika utimamu wake kwani niliikumbuka sana familia yangu.
"Sijaridhia na sipo tayari kuishi na huyu mwanamke"
Nilisema kwa hasira.
Palepale ule umati mkubwa wa watu ukatoweka nikabaki na jini Vumia ambaye alinitazama kwa mshangao uliochanganyika na hasira.
"Umefanya nini wewe binadamu..hakika.."
Kabla hajaendelea kauli yake ilikatizwa.Mbele yetu walionekana mwanamke na mwanaume waliokuwa na umri wa makamo.Sura yao ilinijulisha kuwa walikuwa wazazi wa jini Vumia hasa baada ya kutazama miguuni mwao na kuona kwato.Akiwa amekasirika baba yake jini Vumia alimuonya binti yake na kumuambia kuwa hakukuwepo na ndoa ya jini yeyote inayofungwa bila ya kuwa na maridhiano baina ya wanandoa hao wawili.
"Nadhani umesikia kijana hayupo tayari kufunga ndoa na wewe na ninahisi ulimlazimisha kijana wa watu.Hebu tueleze kijana ulikubali kumuoa huyu msichana au alikulazimisha"
"Sikukubaliana naye jambo lolote,yote aliyafanya kwa kunilazimu na pia,mimi tayari nipo kwenye ndoa na nina mtoto hivyo sipo tayari kuwa naye"
Niliwajibu.
"Basi sawa tumekuelewa.Vumia nadhani umesikia kila kitu,sitaki nione ukimsumbua tena kijana wa watu,amesema hakutaki na ana ndoa.Kwahiyo tafuta ambaye mtaridiana kwa kila kitu"
"Lakini mama"
"Lakini nini?,kwanza ondoka hapa usijekunikasirisha bure"
Aliongea kwa hasira mwanamke huyo na kusababisha jini Vumia atoweke eneo lile akiacha ukelele mkali wakutisha.
Baada ya hapo nilikabidhiwa vijana wawili wa kijini walioagizwa wanirudishe duniani.Walinifikisha mpaka nje ya kile kidimbwi na kuniambia nifunge macho na kufungua baada ya sekunde kadhaa.Nilipofanya hivyo ghafla nilijikuta ndani ya chumba changu.Mke wangu na mwanangu wakiwa bado wamelala ikiwa ni majira ya saa kumi na moja asubuhi.Kwakweli matukio niliyokutana nayo siku hiyo yalifanya niamini kuwa dunia ina mengi ambayo yamefichwa ambayo huenda baadhi yetu wangepata nafasi ya kuyaona,wangeishia kufa kwa mshituko wa moyo.
Kwakweli siku hiyo nilikuwa na furaha sana.Nilijua nimemaliza kila kitu na nisingekumbana tena na kiumbe huyo wa kutisha.
Nilimsogeza vizuri mwanangu na kujilaza.Usingizi ukanipitia.Katikati ya usingizi niliota ndoto ya kutisha.
Nilimuona jini Vumia akiwa chumbani kwangu.Wakati huo mimi pamoja na mke wangu na mwanangu tulikuwa tumelala fofofo.Jini Vumia akainua mkono wake.Shuka lililotufunika likawa likielea hewani.Ghafla jini Vumia akabadilika na kuwa kiumbe wa kutisha.Sura nyeusi sana iliyokuwa na macho mekundu yaliyoiva kama nyanya,kucha na meno vikiwa virefu na ncha kali.Miguu yenye kwato iliyofanana na ya farasi.Vyote viliujenga mwili wake wa kutisha.Akamsogelea mke wangu na kunyoosha mkono.Kisha mkono huko akaukita kwa nguvu katikati ya tumbo la mke wangu.Tumbo likachanwa vibaya kwa kucha zake ndefu.Akanyanyua mkono huo ikiwa sasa ulishika nyamanyama nyingi kutoka katika tumbo la mke wangu lililokuwa wazi likivuja damu nyingi.Katika hali ya kutisha zaidi jini Vumia aliyekuwa akitisha kuliko kawaida akaweka nyamanyama zile mdomoni na kuanza kuzitafuna.Baada ya kumaliza kufanya tukio hilo la kutisha,akanyoosha mkono.Likatokea jeneza dogo lililokuwa saizi ya mtoto mdogo.Jeneza hilo lilikuwa wazi.Taratibu jini huyo akajivuta mpaka  pale kitandani.Akamnyanyua mwanangu na kumshika miguuni.Huku nikishuhudia kwa macho yangu,jini huyo akaingiza kichwa cha mtoto wangu huyo wa pekee.Akaanza kukitafuna mfano wa mtu alaye mnofu mtamu.Damudamu zilitiririka kutoka kwenye kinywa chake.Jini huyo hakujali,akaendelea kumtafuna mwanangu mpaka alipomaliza kichwa chote ikabaki shingo.
Akachukua kiwiliwili cha mwanangu na kukiingiza katika lile jeneza dogo.
"Haya ndiyo malipo yako kwa usaliti uliofanya..Bye tutaonana tena mpenzi".
Aliniambia jini Zainushi na kutoweka na lile jeneza.Papo hapo nikastuka kutoka usingizini.Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio.Mwili ulilowa kwa jasho.Harufu kali ya Marashi ya jini Vumia ilijaa chumba kizima.
Nilipomtazama mke wangu na wanangu walikuwa bado wamelala.Nilipotazama ukutani,nilichanganyikiwa.Saa ilinijuza ilikuwa saa sita mchana.
Mara nikasikia mlango wa nje ukigongwa kwa nguvu mithili ya kutaka kuvunjwa.

Nini kitafuata?.
Tukutane kesho

LIKE NA SHARE. UNAWEZA KUISOMA YOTE KWA KULIPIA BUKU TU.

NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-05

Ilipoishia..

Nilipomtazama mke wangu na wanangu, walikuwa bado wamelala.Nilipotazama ukutani,nilichanganyikiwa.Saa ilinijuza ilikuwa saa sita mchana.
Mara nikasikia mlango wa nje ukigongwa kwa nguvu mithili ya kutaka kuvunjwa.

Endelea..

Kelele nyingi zilisikika kutoka mlangoni.Nilitoka chumbani haraka na kuelekea ulipokuwa mlango na kuufungua.
Kundi kubwa la watu waliokuwa na silaha za jadi lilisimama nje ya mlango wa nyumba yangu.Watu hao walionekana kuwa na hasira mno.
"Si mnasikia na hii harufu ya marashi,haya shindweni kuamini tena sasa,niliwaambia huyu jamaa ni mshirikina"
Alisema mmoja kati ya majirani zangu na kutoa nafasi kwa umati huo mkubwa kunivuta nje ya nyumba yangu kama mwizi na kuanza kunishushia kipigo kikali.Hakika nilishangaa mno,sikujua sababu ya watu wale kunifanyia kitendo hicho cha kikatili.Mbaya zaidi hawakunipa hata nafasi ya kujieleza.Wakati wakiendelea kunipa kipigo baadhi yao waliingia chumbani kwangu na kuitoa miili ya mke wangu na mwanangu ambayo kwa sasa haikuwa na uhai.
"Si niliwaambia huyu jamaa mwanga,ona ameua mke na mwanaye,lazima tumuue huyu kila siku   tunaamka wachovu kumbe wajinga kama hawa ndio hufanya kazi ya kutuchezea,..pia kabisa uwa".
Alisikika tena jirani yangu huyo niliyekuwa nikipatana naye kuliko kawaida.Kwakweli mabadiliko yake ghafla yalinishangaza mno.
Huku damu nyingi zikiendelea kunivuja,nilijaribu kujinasua katikati ya kundi hilo kubwa la watu hasa baada ya miili ya mwanangu na mke wangu ikichukuliwa na kupelekwa nisipopajua,lakini hiyo haikusaidia lolote kwani tofali la kuchoma lilitua katika utosi wangu na kunikata kauli,nilianguka na kupoteza fahamu.
Ghafla nilistuka na kujikuta katikati ya giza nene.Upepo mkali ulivuma na sauti ya mawimbi ya maji ilisikika.
Baada ya kupiga hatua kadhaa niligundua nilikuwa katika eneo la fukwe ambalo ikiwa ni baada ya kukanyaga mchanga laini.Nikiwa bado katika sintofahamu ile,ghafla nilianza kusikia sauti za watu waliokuwa wakiimba.Katika kusikiliza niliweza kutambua walikuwa wakiimba kwa kutumia lugha ya kikabila ambayo sikuweza kuifahamu.Sauti ya watu hao ilizidi kuongezeka baada ya kila sekunde na kufanya niuhusi ukaribu wa watu hao.Cha ajabu sikuweza kuona kiumbe yoyote zaidi ya giza nene.
Huku ngoma za asili zikidundwa kwa nguvu.Kundi hilo kubwa la watu wasioonekana lilizidi kunisogelea na kunizunguka huku zikiimbwa nyimbo pamoja na vicheko vya kutisha.Kijasho chembamba kilianza kuulowesha mwili nikajua huo ndio mwisho wangu.
Nizidi kukushangaza msomaji..pamoja na kipigo kizito nilichokuwa nimepokea kule nyumbani kwangu kilichoacha majeraha makubwa katika mwili wangu ambayo katika hali ya kawaida yangetumia zaidi ya miezi sita kupona huku nikiwa katika uangalizi maalumu hospitali,kwakweli nikiwa pale sikuwa hata na mchubuko ambao labda ungeweza kuwa ushahidi tosha kwamba nilikuwa majeruhi aliyekuwa katika mahutihuti.
Nikiwa bado katika hofu kuu na mshangao ghafla katika sehemu niliyokuwa nimesimama moto mkali ulilipuka na kuanza kunichoma.Kwakweli nilijaribu kwa kila namna kujitoa katika moto huo ambao ulikuwa ukijichocheza kadiri nyimbo zile za asili zilivyokuwa zikirindima eneo lile.
Nilianza kubabuka ngozi ya mwili kutokana na muunguzo wa moto huo.Harufu nzuri ya nyama ya kuchoma ambayo pia ilipenya vema katika pua zangu ilianza kusikika vyema katika eneo lile na kusababisha ngoma pamoja na nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kutulia.
Ghafla nikajikuta katikati ya kundi kubwa la watu waliokuwa kama walivyozaliwa.Wake kwa waume,wakubwa kwa wadogo.Walijipaka rangi mbalimbali katika miiili yao.Watu hao waliokuwa wakinitazama kwa uchu wakiyatumbua macho yao vyema walianza kunizunguka huku wakinusa kama mbwa aliyekumbana na kitoweo mahali fulani.Wakaanza kuimba tena huku wakinizunguka lakini sasa hakukuwa na sauti za ngoma.Moto ule uliendelea kunichoma vyema nikiugulia maumivu makali karibu kufa.Harufu nzuri ya nyama choma nayo ilizidi kushamiri eneo lile.Ghafla ilisikika mingurumo mikali ya wanyama.Watu wale wakaacha njia iliyoniwezesha kumshuhudia binadamu aliyekuwa amepanda fisi wawili waliokuwa wakija mbio kwa kasi.
Walipofika karibu na eneo lile fisi hao wakatoweka mbele ya macho yangu akaonekana mwanamke mzee aliyekuwa uchi wa mnyama.Mwanamke huyo alinitazama kwa macho ya kutisha yaliyoiva kwa hasira kupitiliza.Kama ilivyokuwa kwa wale wengine,mwanamke huyo naye hakuwa amejisitiri kwa chochote.
"Mama mkwe?"Nilijikakamua na kuongea kwa mshangao.
Kikafuata kicheko kizito kilicho ambatana na radi kali.
"Unashangaa nini wewe shwaini.Kwa tamaa ya mali umeshirikiana na majini ukamtoa mwanangu kafara.Sasa nikuambie tu,leo hapa huchomoki na utaliwa nyama na wananzengo ukiwa unashuhudia hivihivi"
Alizungumza mama mke wangu ambaye alikuwa ndiye mama wa mke wangu.
Najua utajiuliza ilikuwaje nikapata uwezo wa kuongea wakati nilikuwa nikiteketea katika moto mkali.Ni kwamba kile kilikuwa kiini macho tu.
Baada ya mama mkwe wangu kuzungumza maneno yale ghafla ule moto ulizima sasa nikajikuta katika mikono ya watu wale niliowatambua kama wanga au wachawi ambao sasa walianza kunipaka udenda mzito uliokuwa ukitoka katika vinywa vyao.Udenda huo ulitoa harufu mbaya mno,na kupelekea nihisi kutapika.Kila nilivyozidi kupakwa uteute huo ndivyo nilivyozidi kuishiwa na nguvu kiasi cha kulegea kupitiliza.Hatimaye nilibaki kama zezetea katikati ya kundi lile na kuanza kuteremsha udenda kama taira.
Mama mkwe wangu mwanga akanisogelea na kupishwa na ule umati wa nzengo ya wachawi.Akanishika sehemu ya paja langu iliyokuwa wazi ambayo iliteleza kwa kupakwa udenda,akapitisha kucha yake iliyokuwa na makali mithili ya wembe mkali.Huwezi amini kucha hiyo ya mwanamke huyo ikakata pande kubwa la nyama katika paja langu.Akanyoosha mkono kikatokea kibuyu kilichoikinga vyema damu yangu.Baada ya kibuyu chake kujazwa  pomoni mama mkwe akaingiza pande la mnofu wa nyama ya paja langu mdomoni na kutafuna,kisha akapiga funda kubwa la damu yangu.
Akapanua mdomo wangu na kuuweka mnofu aliokuwa ameabakiza kisha akaniamuru kutafuna.Bila kujitambua nilianza kuitafuna nyama ile iliyotoka katika mwili wangu ambayo ilikuwa na hali ya chumvichumvi mno.
Ukelele mkubwa wa shangwe ukalipuka.Mama mkwe akasogea na kibuyu chake kilichojaa damu akakaa juu ya paka mkubwa mweusi aliyekuwa amejilaza pembeni akaendelea kupiga funda za ile damu.
Kuondoka kwa mama mkwe kuliachia nafasi  kwa wachawi wengine kula chakula pendwa kabisa miongoni mwa watu wa giza.
Wachawi hao wakanivamia na kuanza kunikata sehemu mbalimbali za mwili wangu kwa makucha yao yenye ukali.
Ghafla kikasikika kicheko kikali mno.Kicheko hicho kikamtisha kila mchawi aliyekuwa katika eneo lile la fukwe za coco beach.Mama mkwe wangu aliyekuwa akiendelea kula mnaofu laini kutoka kwenye paja langu alisitisha zoezi hilo na kusimama.

Nini kitafuata.Usikose ijayo.

UNAWEZA KUSOMA STORY YOTE KWA BUKU TU NICHEKI 0629980412

NILIKIONA CHA MOTO-06


Ilipoishia..

Mama mkwe wangu mwanga akanisogelea na kupishwa na ule umati wa nzengo ya wachawi.Akanishika sehemu ya paja langu iliyokuwa wazi ambayo iliteleza kwa kupakwa udenda,akapitisha kucha yake iliyokuwa na makali mithili ya wembe mkali.Huwezi amini kucha hiyo ya mwanamke huyo ikakata pande kubwa la nyama katika paja langu.Akanyoosha mkono kikatokea kibuyu kilichoikinga vyema damu yangu.Baada ya kibuyu chake kujazwa  pomoni mama mkwe akaingiza pande la mnofu wa nyama ya paja langu mdomoni na kutafuna,kisha akapiga funda kubwa la damu yangu.
Akapanua mdomo wangu na kuuweka mnofu aliokuwa ameabakiza kisha akaniamuru kutafuna.Bila kujitambua nilianza kuitafuna nyama ile iliyotoka katika mwili wangu ambayo ilikuwa na hali ya chumvichumvi mno.
Ukelele mkubwa wa shangwe ukalipuka.Mama mkwe akasogea na kibuyu chake kilichojaa damu akakaa juu ya paka mkubwa mweusi aliyekuwa amejilaza pembeni akaendelea kupiga funda za ile damu.
Kuondoka kwa mama mkwe kuliachia nafasi  kwa wachawi wengine kula chakula pendwa kabisa miongoni mwa watu wa giza.
Wachawi hao wakanivamia na kuanza kunikata sehemu mbalimbali za mwili wangu kwa makucha yao yenye ukali.
Ghafla kikasikika kicheko kikali mno.Kicheko hicho kikamtisha kila mchawi aliyekuwa katika eneo lile la fukwe za coco beach.Mama mkwe wangu aliyekuwa akiendelea kula mnaofu laini kutoka kwenye paja langu alisitisha zoezi hilo na kusimama.

Endelea..

Ghafla likaonekana joka kubwa la kijani lililokuwa na kidani kilichong'aa sana kichwani.Hakika joka hilo lilikuwa kubwa sana.
Lilitoa sauti kali ya kupuliza likapanua kinywa chake kilichokolezwa kwa wekundu ndani.Meno mawili yaliyochongoka sawia yalionekana.
Kwa madaha joka hilo likaanza kuwafuata wale wachawi.Cha ajabu lilinipita na kunitazama kwa macho ya upole.
Huwezi kuamini nilishuhudia joka lile likiwameza wale wachawi.
Nilibaki nikitetemeka mithili mtoto mdogo aliyeachwa ndani ya nyumba pekee wakati wa usiku mnene.Joka lile liliendelea kuwameza wale wachawi katika taswira ya kutisha sana.
Halikuwameza wote.Alibaki mkuu wao ambaye ndiye mama mkwe wangu.
Joka hilo lilimtazama kwa macho yaliyoiva kwa hasira kisha likamtemea uteute mwingi wa kijani.Palepale yule bibi akapotea na sikuweza kuliona tena lile joka.
Nilibaki nimekaa pale chini katikati ya msitu mnene,hofu na maumivu vikiniandama.
Hakika nilikuwa katika hali ya kukata tamaa.Nilishindwa kujua kabisa hatima yangu.Sikuwa na familia tena mke wangu na mwanangu waliondolewa duniani katika mazingira ya kutatanisha.
Kila kilichoonekana mbele yangu,kilikuwa mauzauza tu.Kama ni maisha sikuwa nayo tena.Kazi sina,hela sina familia sina mbaya zaidi ni hali ya hofu iliyokuwa imenitawala.Nilijikuta nikizidisha chuki dhidi ya jini Vumia.Kila nilipokumbuka machungu aliyokuwa amesababisha katika maisha yangu ni machozi tu yaliyosaidia kuipoza hasira niliyokuwa nayo.
Nilijinyanyua pale chini na kuanza kutembea kama mlevi wa pombe kali.Hakika nguvu ziliniisha.
Nilitembea kwa hofu sana nikitazama huku na kule.Kila hatua niliyopiga nilihisi kama lile joka la ajabu likija nyuma yangu tayari kunifanya kitoweo.
Mvua nayo haikuwa mbali ilikamilisha mauzauza yale kwa kuanza kunyesha ikiambatana na radi kali.Niliendelea kutembea nikielekea nisipopajua.
Baada ya mwendo kama wa saa nzima nikipata surubu ya mvua na baridi kali bila kusahau hali ya hofu iliyokua niseme imeniathiri kisaikolojia.Ghafla kwa mbali niliona mwanga mkali wa taa.
Kisha ukasikika mlio wa gari.
Mungu si athumani.Mbele yangu lilionekana gari dogo aina ya Noah likija taratibu.
Katika barabara mbovu katikati ya pori lile gari hilo lilipambana na madimbwi yaliyojaa maji.
Nilijisogeza katikati ya barabara kuomba msaada nikiweka nadhiri iwapo dereva wa gari hilo angekataa kusimama, basi ningekuwa radhi anigonge kabisa.
Kama nilivyo tarajia gari hiyo iliponifikia ilisimama kisha kioo cha gari kikafunguliwa.
Nikasikia sauti ya kike ikiniita.
"We kaka kuna nini mbona peke yako katikati ya pori lote hili"
Sauti laini ya ilizungumza na kufanya nisogee kilipokuwa kioo cha upande wa derava.
Macho yangu yalipigwa na butwaa baada ya kukutana na sura ya msichana mzuri kuliko wote niliowahi kuwaona maishani.
Kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kupenyeza ndani ya gari kabla hata sijajibu msichana huyo aliniagiza kuingia ndani ya gari.Nilifungua mlango wa gari ile na kukaa katika siti za nyuma.
Hapo yakafuata maongezi ya muda mrefu kati yangu na msichana huyo aliyeonyesha kuhuzunishwa na simulizi yangu.
Sikutaka kumuambia juu ya matukio ya kimazingara niliyokumbana nayo kwa kuhofia msichana huyo angeweza kunitelekeza akinihisi mwanga.
Nilimwambia nilitekwa na watu walionitelekeza katika lile pori.
Kwa upande wake yeye aliniambia alitoka kijijini kwao kuisalimia familia yake bahati mbaya gari ilipata tatizo katikati ya pori na kusababisha achelewe.
"Ndio hivyo sa hivi naelekea nyumbani,sijui kama kesho nitaweza kuwahi kazini"
Aliniambia msichana yule.
Safari iliendelea mpaka yalipotimia majira ya saa kumi na moja alfajiri.Ni wakati huo tuliiingia ndani ya jiji la Dar.
"Asante kwa kunifikisha hapa dada yangu.Alaah akujalie baraka."
Nilimwambia yule dada nikiomba asimamishe gari nishuke,lakini yule dada alisimamisha gari akanitazama kwa muda kwa macho ya upole na kuniambia.
"Kweli unataka uondoke na hali hiyo uliyokuwa nayo?,Mimi naomba tu nikusaidie ukaishi kwangu nikupeleke hospitali ukapate matibabu maana hata afya yako inaonekana haijkaa vizuri.Tafadhali naomba unipe nafasi ya kukusaidia."
Aliniambia msichana huyo katika hali ya  kunionea huruma na msisitizo.
Niliona nisiendelee kuweka ugumu nilikubaliana na msichana huyo.
Tukafika mpaka nyumbani kwake iliyokuwa katika maeneo ya Mbezi beach ambapo nilishangaa sana baada ya msichana huyo kuniambia alikuwa akiishi peke yake katika nyumba hiyo ya kifahari na akiwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Kwa kweli nyumba ile ilikamilika.Ilikuwa na kila hadhi ya kuitwa nyumba ya kifahari.
Kingine alichonistaajabisha msichana huyo ni kitendo cha kuniambia hakuwa na mwanaume yaani hakuwa ameolewa.Mshangao wangu ulitokana na muonekano wa kuvutia aliokuwa nao ambao kwa kawaida lazima vijana wengi wangekuwa wameshatupa ndoano zao na kumnasa.
Jioni baada ya kujiandaa vizuri msichana huyo alinipeleka hospitali ambapo nilipata vipimo na kugundulika kuwa na homa nikapatiwa madawa na kurejea nyumbani.
Huko nyumbani nilikuwa nikiishi na msichana huyo mrembo kabisa aliyebarikiwa kila kona.
Yeye alikuwa akiondoka asubuhi na kurudi jioni lakini hakuwahi kunitamkia kazi aliyokuwa akifanya.Tuliishi kama kaka na dada lakini sikuzote nilikuwa mtu wa mawazo mno.Niliiwaza sana familia yangu.Ile hali ya hofu nayo ilizidi kuniandama,sikuwa na amani kabisa.Cha kushangaza kila wakati niliokuwa nimezama sana katika mawazo,usingizi mzito ulinipitia nakuota ndoto nikiwa na jini Vumina katika sehemu nzuri iliyotulia,tukiwa katika hali ya mahaba.Kama wapenzi wa muda mrefu.Jini huyo hakuacha kunitamkia kuwa alikuwa akinipenda sana na aliniambia nisihofu kuhusu familia yangu kwani ilikuwa salama.
Pia wakati wa usiku nilipolala mara nyingi nilisikia mlango ukifunguliwa kisha akaonekana jini Vumia akija kitandani na kufanya mapenzi na mimi.Nilipo amka asubuhi kweli nilihisi harufu ya manukato ya jini huyo ikiwa katika mwili wangu.
Matukio hayo yalizidi kuniongezea msongo nikawa mtu wa kuwaza sana.Hali hiyo aliiona yule msichana nilikuwa nikiishi naye ambaye na kunionya nisiwe mtu wa kuwaza sana.
Maisha yaliendelea hatimaye baada ya siku nyingi kupita nilijikuta nikisahau matukio yote ya nyuma na ile hali.ya msongo na hofu ikapotea.Sikumuona tena jini Vumia katika ndoto yangu.
Maisha ya utulivu na maelewano niliyoishi na msichana yule.Yalianza kuibua hisia fulani kati yetu.
Haikuchukua muda kwetu kugundua hilo.Tukajikuta tumewekana wazi juu ya yaliyokuwa mioyoni.
Ndipo likachipuka penzi kati yetu penzi lililozaa ndoa ambayo ilikuwa makubaliano yetu wawili tuliokuwa tukiishi pamoja.
Nilianza kuishi na Zainabu kama mke wangu.Akanifungulia biashara nikaanza kujituma.
Siku zote sikuwahi kujua mahali mke wangu Zainabu alipofanyia kazi zaidi ya kukutana nyumbani usiku baada ya kazi.
Hakutaka pia kunieleza kuhusu familia yake.Hayo yakasababisha maswali mengi kichwani kwangu.

Itaendelea..

NJOO WATSAP USOME MPAKA MWISHO KWA BUKU.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad

Hollywood Movies