( 1–3 )
🔥📚
NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-01
Anza na uhondo huu..
Ilikuwa ni kazi ambayo niliipenda sana.Sio kwamba ilikuwa kazi bora,bali ni kwa jinsi ilivyonisaidia kujikimu na kuhudumia familia yangu.
Ingawa nilifanya kazi katika mazingira magumu,sikujali baridi kali ya usiku pamoja na kitendo cha kumuacha mke wangu mpweke kitandani ambapo sikujua waliofanya kazi ya kumpa joto mke wangu usiku.
Naam,nilifanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja huko Kilwa iliyomilikiwa na mhindi.Muda wangu wa kazi ulikuwa ni usiku.Ni mimi niliyechagua kulinda usiku kwani ilikuwa rahisi kwangu kujihusisha na shughuli nyingine wakati wa mchana.Lindo lenyewe lilikuwa la mtu mmoja yaani usiku mzima nililinda peke yangu.
Siku moja nikiwa katika lindo ikiwa majira ya saa saba na nusu usiku,mvua iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha.Mvua hiyo ilipelekea umeme kukatika.Niliwasha tochi yangu kubwa na kujikunyata katika kibaraza kilichokuwa nje ya geti la kuingilia ndani ya kampuni.Hakukuonekana kiumbe yeyote nje,ilisikika sauti ya manyunyu yaliyokuwa ya kiyachapa mabati ya nyumba mbalimbali,radi nayo ilichukua hatamu.
Kwa kuwa baridi ilizidi sana nilikaa kwenye kigoda na kujikunja ndani ya koti langu zito.
Ilipofika majira ya saa nane usiku hivi mvua ikiendelea kunyesha,ghafla nilisikia sauti za hatua za mtu aliyekuwa akikanyaga maji.Nilistuka nikanyanyua gobole langu na kuwasha tochi.
Mbele yangu alionekana msichana mrefu kiasi mweupe na aliyekuwa na nywele ndefu laini zilizo lala vizuri.Msichana huyo alinipishana na mimi na kuingia pale kibarazani.
"Kaka naomba unisaidie koti lako,nimechelewa nyumbani kesho ntakurudishia"
Aliniambia msichana huyo aliyekuwa akitetemeka kwa baridi kutokana na kuvaa kigauni chepesi cheusi kilicho acha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.
"Unatoka wapi usiku huu dada yangu,na unaelekea wapi na mvua hii"
"Siendi mbali nimeshafika nimebakiza kama nyumba mbili nifike"
"Sawa, lakini nikikupa koti langu inamaana nipigwa na baridi mpaka asubuhi"
"Naomba unisaidie tu kaka yangu,usijali kesho ntakuletea zawadi yako"
Kutokana na huruma yangu nilimpa koti langu bila kujua matatizo yaliyokuwa mbele yangu.
Nilibaki kumtazama msichana huyo mpaka alipotokomea gizani kwa kuwa alinikataza kummulikia.
Cha kushangaza mpaka inafika asubuhi sikuhisi baridi kabisa.Wala sikuwaza kuhusu lile koti.
Kesho yake usiku majira yale yale ya saa nane,yule dada alipita tena.Wakati huu alikuwa amevaa lile koti langu.Cha ajabu wala hakupokea salamu yangu nilipomsalimia,alinipita na kuendelea na safari.Nilijiuliza sana kuhusu tukio hilo nikaamua kumfuata mpaka atakapoishia ilimradi anipatie koti langu.
Nilipiga hatua ya kwanza..ya pili..kisha ya tatu..ghafla umeme ukakatika.Nikasimama na kuingiza mkono katika koti langu nitoe tochi lakini kabla hata sijafanikiwa kuitoa,umeme ulirudi na sikumuona tena yule msichana.Sikutaka kukubali aondoke kirahisi hivyo,nilipiga hatua za haraka kuelekea njia aliyoelekea.Kwa mbali nilimuona akiingia ndani ya jumba fulani ambalo halijakamilika.Yaani ilikuwa nyumba ya bloku ambayo haijapauliwa wala kuwekewa milango na madirisha.
Kwa haraka nikachukua hatua na kulifikia lile jumba.Nikaingia ndani huku nikimulika na tochi yangu.Ghafla tochi ilizima kukatawala kiza nene.Kahofu kakanishika kutokana na tukio hilo la kustukiza.Ila nikapiga moyo konde na kuingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa kimepakana na sebule.Macho yalinitoka baada ya kuona kitu cha ajabu kabisa maishani mwangu.Niliona mtu mrefu sana ambaye nilipotazama juu sikuweza kuuona uso wake.Miguu ya kiumbe huyo ilifanana na miguu ya ng'ombe ama niseme punda kutokana na kuwa na kwato.
Nilianza kutetemeka mpaka nikawa naisikia miguu yangu.Mkojo ulinitoka baada ya kusikia sauti kubwa ya kicheko cha kike ambayo ilinijulisha kuwa kulikuwa na zaidi ya mchekaji mmoja.
Nilijibaraguza na kutoka mbio kama mwizi anayekimbizwa sokoni.
Nilipofika kazini,nilishindwa kuamini kwa nilichokiona.Geti la kuingilia ndani ya stoo lilivunja,ndani ya stoo kulikuwa patupu haikuonekana hata punje ya mchele japo mwanzo kulikuwa na shehena kubwa ya gunia za mchele.
Nilihisi kuchanganyikiwa nilitembea huku na kule kama kichaa.Nikachukua simu na kumpigia meneja wa ile kampuni.
"Bosi naomba ufike hapa,sasa hivi kuna tatizo limetokea"
"Tatizo gani tena usiku huu,mbona unakuwa msumbufu"
"Naomba tu ufike mengine tutazungumzia hapa"
Dakika ishirini baadae meneja alifika akiwa ameambatana na makachero watatu.
Niliwaeleza kila kitu na kuwaonyesha stoo iliyokuwa tupu pamoja na mpango wa grili uliokuwa umevunjwa.
Lakini nilipigwa na butwaa baada ya kukuta geti likiwa zima kabisa na kufuli imefunguliwa na kuwekwa pembeni ya mlango.
Ndani ya stoo kulikuwa patupu kabisa tena kwa sasa pasafi mno.
"Hivi wewe unaakili kweli"
"Umesema umevamiwa,umeumizwa wapi,ukasema grili limevunjwa mbona zima kabisa.Haiwezekani huu wizi umepanga sasa unajidai umevamiwa"aliniambia meneja.
"Kwa kweli nilivamiwa na hili grili lilivunjwa nikishuhudia kwa macho yangu"nilijitetea huku hofu imenitawala.
Lakini nilinyamazishwa na kofi zito kutoka kwa mmoja wa kachero aliyenituhumu moja kwa moja kama muhusika mkuu.Nilipigwa pingu mikononi na kupelekwa kituo cha polisi.Nikatupwa sero mpaka jua lilipo wia.
Asubuhi na mapema uongozi wa ile kampuni ulifika pale kituoni na kusomewa maelezo yangu ambayo kutokana na ushahidi yalinifunga moja kwa moja kama mshitakiwa mkuu.Wakati hayo yakiendelea nje ya dirisha la ofisi ya kituo cha polisi kwa mbali nilimwona yule msichana akikatiza barabarani aligeuka na kutazamana nami kisha akaonyesha tabasamu.
Ilipangwa siku ya kesi kusomwa na ilipofika siku hiyo familia yangu ilifika pale mahakamani pamoja na uongozi wote wa ile kampuni nikasomewa mashitaka na kwa kuwa kulikuwa na vithibitisho vyote ,hakimu aligonga meza kwa rungu lake na kutoa hukumu ya miaka thelathini na faini ya shilingi milioni tano.Au nilipie gharama ya mali zote zilizopotea iliyokadiria milioni thelathini.
Hukumu hiyo ilikuwa msumari wa moto kwangu mimi na familia yangu ya mke mtoto mmoja.Ilikuwa ngumu kuweza kulipia zile gharama hivyo moja kwa moja nilijua naenda kunyea ndoo.
Baada ya hakimu kumaliza kutoa hukumu hiyo ghafla alinyanyuka mmoja wawatu waliokuwa wakisikiliza ile kesi.Nilipomtazama vizuri,niligundua alikuwa yule msichana niliyempatia koti langu usiku.
Nilistuka! mapigo ya moyo yakanidunda kwa kasi.
Mwanamke yule alifika mpaka mbele ya mahakama na kuzungumza.
Je nini kitaendelea? Usikose kisa hiki cha kweli kabisa.
Like na share.
Story hii inapatikana Yote Watsapp kwa shilingi 1000/= tu utasoma mpaka mwisho .
Itaendelea..
NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-02
Ilipoishia..
Alifika mpaka mbele ya mahakama na kuzungumza.
Endelea..
Salam mutukufu hakimu.Naomba unipe nafasi ya mwisho nitoe utetezi kwa huyu kijana.Kulingana na niliyoyaona,nadhani mkisema moja kwa moja huyu amekula njama na majambazi mnakosea.Ni kwamba leo asubuhi na mapema sana wakati naelekea kwenye shughuli zangu niliona gari ndogo aina ya toyota iliyokuwa imesheheni magunia ya mchele ikipaki nje ya nyumba fulani hapo mtaa wa mnazi.Nisiseme moja kwa moja kuwa hao ndiyo watuhumiwa lakini ningeomba kwanza muwafuatilie ndipo baada ya uchunguzi hukumu itolewe"
Alimaliza msichana yule maneno ambayo yaliungwa mkono moja kwa moja na kila aliyekuwa katika chumba cha mahakama.
Hakimu aliatoa amri nirudishe rumande ambapo kikosi cha upelelezi cha polisi kiliondoka kuelekea katika jengo ambalo waliagizwa na yule msichana wa maajabu.
Huko rumande kutokana na uchovu mwingi nilikaa na kujiegemeza ukutani usingizi ukanichukua.
Papo hapo niliota ndoto nimekutana na yule msichana nje ya jengo la mahakama.
"Kwanini ulinifuata?"aliniuliza msichana huyo aliyekuwa amejisitiri kwa ushungi akiweka mtindo wa kiarabu.Midomo yake aliipamba kwa wanja wa bluu na nyusi zake akizipamba kwa wanja mweusi hali iliyomfanya azidi kuvutia.
"Kwasababu nilihitaji koti langu"
"Sawa tuachane na hayo wakikuuliza unawajua hawa watu,waambie unawafahamu na ndio waliovamia usiku"Aliniambi yule msichana na kunionyesha wanaume saba waliokuwa wamesimama pembeni yake.
Nilimuitikia kwa kutingisha kichwa ambapo papo hapo,nilistuka usingizini na kujikuta nikiitwa na mmoja wa polisi.
Nilijinyanyua pale kichovu lakini kichwani yakabaki mawazo kuhusu ile ndoto niliyotoka kuota muda mfupi uliopita.
"Unawafahamu watu hawa"aliniuliza polisi na kunikumbusha maneno ya yule msichana aliyoniambia ndotoni.
Nikakubali na kuwaambia ndio waliofanya uvamizi usiku huo.Kama nilivyoona ndotoni sura na idadi ya wanaume wale haikuwa tofauti.
Askari aliandika maelezo na kuyakabidhi ofisini kisha ilipotimia saa saba mchana tuliitwa tena mahakamani ambapo katika kuchunguza sikuweza kumuona tena yule msichana.
"Bwana Lameck kutokana na uchunguzi tuliofanya,tumefanikiwa kukamata wahusika wa tukio la wizi hivyo kuanzia sasa upo huru hauna mashitaka yoyote,ila kabla ya kuondoka utatakiwa ufike ofisini kwa mazungumzo machache"Alisema hakimu kauli iliyoibua furaha katika moyo wangu.Nilipomtazama mke wangu niliona akilia machozi ya furaha.
Baada ya kumaliza taratibu zote niliachwa huru lakini niliporudi kazini nilipewa barua ya kufutwa kazi.Hapo nikapata mtihani mwingine wa kutafuta kazi.
Nikaandika barua na kutuma kwenye makampuni mbalimbali ya ulinzi ambapo nilitegemea nisingeweza kukosa hata kampuni moja ambayo ingenihitaji. Karibu kila ofisi niliyotuma barua ya maombi majibu yalikuwa yaleyale hakuna kazi.
Nilikaa na mke wangu tukajadili kwa kuwa tayari nilishakata tamaa hivyo nikatafuta ushauri kwa mke wangu kujua ni shughuli gani nyingine ambayo ningeweza kufanya angalau isaidie kupatikana kwa sukari.Mke wangu hakunikatisha tamaa,alinipa moyo niendelee kutafuta kazi hiyohiyo ya ulinzi kwani ndiyo niliyokuwa na uzoefu nayo zaidi.Nakuhusu maisha tusingekwama kwani yeye angeendelea kupata pesa kidogo kutoka katika kazi yake ya genge la mbogamboga.
Licha ya yote yaliyonikuta sikumwambia mke wangu kuhusu yule msichana wa maajabu.Nilijua kufanya hivyo huenda kungezusha mapya ambayo huenda yasingekuwa mema.
Kabla ya kulala siku hiyo nilimuita mke wangu sebuleni tukasoma bibilia na kusali.Nilitegemea kwa uwezo wa mwenyenzi mungu ningefanikiwa kupata kazi.
Ingawa nilikuwa nimesongwa na mawazo mengi ya kuachishwa kazi pamoja na kumbukizi za kutisha za yule msichana,sikuchelewa kupata usingizi ghafla usingizi mzito ulinipitia.Nikazinduka usiku mwingi.Nikahisi kama kulikuwa na mtu ananiita.Nikatega masikio yangu na kusikiliza.Kulipita ukimya kidogo kisha nikasikia tena sauti ikiita jina langu.Ilikuwa sauti ya kike niliyoitambua.Lakini sikuweza kukumbuka mara moja ilikuwa ya nani na alikuwa wapi.
"Lameck!Lameck!"sauti hiyo iliendelea kuita.Moyo ulishituka.Nikaendelea kusikiliza kwa makini.Niligundua sauti hiyo ilikuwa ikitokea mlango wa nje yaani geti.Lakini ni nani huyo ananiita usiku huu?,nilijiuliza bila kupata jibu.Sauti hiyo ilitulia kwa muda kisha ikasikika tena ikiwa sasa aliyekuwa akiita alianza kubisha hodi.Hapo akili yangu ikazinduka. Nikakumbuka ni sauti ya yule msichana niliyemuazima koti.
"Amejuaje sehemu ninayoishi na anataka nini usiku huu"nilijiuliza tena bila kupata majibu.
Nikatazama pembeni yangu nikawaona mke wangu na mwanangu wakiwa wamelala fofofo.'Ataitana atabisha mpaka watu wa toke na hakika mimi sitatoka'nilijiambia.
Na ukweli aliita mpaka ile sauti ikapotea ukimya ukatawala.
Sikupata tena usingizi mpaka asubuhi.
Siku ya pili majira yaleyale nilisikia tena.
"Lameck!Lameck!"
Nikastuka usingizini lakini nilipigwa na bumbuwazi baada ya kujikuta kitandani peke yangu.
Safari hii alibisha na kuita mara chache tu kisha nikasikia mlango wa nje ukifunguliwa.Hakika nilistuka.Lakini nilijipa moyo nikajua huenda akawa mke wangu kwa kuwa sikumuona kitandani nikahusi labda alimpeleka mtoto uani.Baada ya mlango huo kufunguliwa nilisikia sauti za viatu zenye visigino virefu vilivyotoa mlio wa ko! ko!ko! huko sebuleni.Punde tu nikasikia mlango wa chumba changu unabishwa huku ile sauti ikiita jina langu. "Lameck Lameck!"sauti ilikuwa ileile ya yule msichana wa maajabu.Moyo ukanienda mbio mpaka nikahisi ulitaka kuchomoka.Ni baada ya kukumbuka nilikuwa peke yangu pale kitandani bila uwepo wa mke wangu na mwanangu niliolala nao kitanda kimoja.Kwa hofu nilijifunika na shuka mwili mzima bila kuacha hata sehemu ya kutazamia.Aliendelea kubisha kwa kitambo kidago kisha baada ya kuona sifungui nikasikia akiondoka.
Tofauti na jana yake,palepale usingizi ulinichukua na nilipokuja kuzinduka ilikuwa majira ya saa tatu ambapo mke wangu alikuwa akinikaribisha kifungua kinywa.Kwa kweli nilishangaa kumuona mke wangu tena akiwa mzima wa afya ilihali usiku sikumuona kitandani.
"Issa yuko wapi"
"Amesha kwenda shuleni"
Alinijibu mke wangu kidogo hofu yangu ikapungua.
Mchana wa siku hiyo nilifunga safari na kwenda kwa mchungani katika kanisa nililosali lengo likiwa kumueleza juu ya masaibu ya kutisha yaliyonikuta yakitokana na yule msichana.
Wakati naingia kwenye wigo wa kanisa niliona msichana amesimama pembeni ya lango la kanisa akiniangalia kwa macho makali huku amekunja uso.Nilipomuangalia vizuri niliona alikuwa yule msichana wa ajabu.Nikageuza shingo yangu nikajifanya sijamuona nikatoka nje ya ua wa kanisa ,lakini nikapata dukuduku la kumwangalia.Niligeuka nyuma kumtazama.Nikaona akinionyesha ishara ya kuniita."Njoo"
Alitamka kwa sauti ya chini akifanya kama aliyekuwa akisikika.Nilipooona ananiita niligeuza uso wangu na kuendelea kwenda.Lakini sikufika mbali niligeuka tena na kuendelea kwenda."Nimekuambia njoo"akaniambia bila kutoa sauti.Sikumtilia maanani niliendelea kwenda.Sasa nilimuona katikati ya lango amesimama akinipungia mkono.Alipoona nazidi kwenda alisimama akanitazama kwa macho ya upole,akiniangalia kwa huruma kama kiumbe kisicho na hatia.Hapo nikapata nafasi ya kuyaona macho yake makubwa ya mviringo yaliyorembwa kwa wanja mweusi hakika alivutia.
Wakati nakwenda huku naangalia nyuma nilimkumbuka mtu aliyekuwa akiniita.Nikageuka haraka na kumuomba msamaha.Kumbe alikuwa ni yule mchungaji.
"Usijali endelea tu"
"Nilikuwa na safari ya kwako"
"Mimi nilikuwa natoka lakini nitarudi kwa ajili yako"
"Nashukuru baba mchungaji nina matatizo makubwa"
Mchungaji alinipeleka katika ofisi yake nikamueleza kisa kizima tangu kukutana na yule msichana kwa mara ya kwanza mpaka tukio la mwisho la kumuona nje ya lango la kanisa.
Papo hapo tukatoka na yule mchungaji kumuangalia yule msichana ambaye hatukufanikiwa kumuona.
Mchangaji akataka nimpeleke mahali yalipokuwa makazi ya yule msichana ambapo nilimpeleka katika lile gofu na kabla ya kuingia alisali kisha tukaingia.
Hatukukuta kitu chochote cha tofauti zaidi ya majani yaliyojiotea eneo kubwa la ndani ya gofu hilo.
Baada ya kuhakikisha hakukuwa na jambo lolote lisilokuwa la kawaida,mchungaji alipibariki na kunipa aya ambazo nilitakiwa kuzisoma kabla sijalala.
Usiku wa siku hiyo majira ya saa nane tena nilistuka.
Nini kitafuata? Usikose ijayo.
NILIKIONA CHA MOTO KAZI ZA USIKU-03
Ilipoishia..
Baada ya kuhakikisha hakukuwa na jambo lolote lisilokuwa la kawaida,mchungaji alipibariki na kunipa aya ambazo nilitakiwa kuzisoma kabla sijalala.
Usiku wa siku hiyo majira ya saa nane tena nilistuka.
Endelea..
Ni baada ya kusikia mlango wa nje ukifunguliwa.Nilipotazama pembeni yangu sikumuona mke wangu wala mtoto wangu,nilikuwa kitandani peke yangu.
Ukasikika ule mlio wa Ko!Ko! kisha nikasikia mlango wa nyumba ukifunguliwa.Zikasikika hatua zikipigwa kuelekea chumbani nilipokuwa nimelala.Hofu ikazidi kunijaa.Kijasho kikaanza kunitoka.
Nikiwa katika taaruki mlango wa chumbani ukafunguliwa.Mbele yangu alionekana yule msichana wa ajabu amesimama.Kwakweli nilishindwa kujua alipopata funguo za kufungua milango yote ile mpaka kunifikia chumbani.Harufu kali ya mashari ilikizaja chumba kizima.Msichana huyo huku akinitizama kwa huruma alichukua hatua na kukaa katika stuli iliyokuwa karibu na kitanda.Wakati huo nilikaa kitandani huku natetemeka.
"Jina langu vumina ni msichana kutoka falme ya kijini,niliyetokea kuvutiwa na wewe.Kifupi nimetokea kukupenda,nahitaji uwe mume wangu"
Alizungumza msichana huyo maneno yaliyozidi kunitisha nikahisi roho ilitaka kuchomoka,hasa baada ya kujitambulisha kama jini.
"Hahha...pana,haiwezekani,shiindwa kwa jina la..yesuu ."Nilisema huku nikisogea pembeni.
Msichana huyo baada ya kuona namkwepa alikuja kukaa kabisa kitandani hapo nikaona nisipofanya jambo ningeweza kufia pale ndani.Nilijinyanyua na kutoka nduki nikiwa nimevaa chupi pekee.Moja kwa moja nikakimbilia katika chumba cha mpangaji mwenzangu ambaye alikuwa rafiki yangu wa muda mrefu.
"Juma,naomba unifungulie kaka"niligonga kwa pupa huku hofu imenijaa.
"Kuna nini usiku huu ndugu yangu"alijibu Juma akiendelea kufungua mlango.
"Acha tu kaka,fungua yote tutaongelea ndani"
Juma alifungua na kupigwa na mshangao baada ya kuniona uchi,Nilimpiga kikumbo na kuingia ndani kwake haraka.
"Mbona hofu na vurugu kaka,na shem na mtoto wako wapi"?aliniuliza Juma.
Hapo nilimueleza kisa kizima kuanzia siku ya kwanza kukutana na huyo mwanamke mpaka hatua ya kuamka usiku na kushuhudia milango ikifunguka na mwisho ni swala la msichana huyo kujitambulisha kama jini.
"Kaka huu mtihani,subiri kesho ikifika tutaongea sa hivi rudi chumbani kwako maana hii inatakiwa iwe siri mkeo asijue chochote"
Juma alimaliza kwa kuniambia hivyo,akanisindikiza mpaka chumbani ambapo katika hali ya kushangaza nilimkuta mke wangu na mwanangu kitandani wamelala jini Vumi hakuonekana wala ile harufu ya marashi sikuisikia tena.
"Usikute ulikuwa unaota kaka,mbona kila kitu kipo sawa wala hakuna mtu yeyote zaidi ya mkeo na mwanao"
Aliniambia Juma.
"Kaka nina uhakika kabisa haikuwa ndoto ni mbambo yaliyotokea nikishuhudia"nilimjibu.
Kesho yake asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa nilimpitia rafiki yangu Juma aliyeniambia kuna njia ambayo ingeweza kumaliza matatizo yangu.
Tulipanda gari iliyotufikisha mtaa wa pili ambapo huko kulingana na maelezo ya Juma kulipatikana mganga aliyesifika kwa kuwa kiboko ya majini.Alikuwa mzoefu sana wa kazi hiyo na alisaidia watu wengi.
"Hapa ndiyo penyewe sasa kaka.Leo nimekuleta upaone ili kesho ujipange uje na hiyo shilingi elfu saba ambayo sikuzote ndiyo gharama ambayo mganga huyu hutoza"aliniambia Juma safari yetu ikaishia hapo hivyo nikarudi kwa ajili ya kujipanga.
Kesho yake asubuhi na mapema nilifika kwa yule mganga huku shilingi elfu saba ikiwa tayari mfukoni mwangu.
Kwa kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa katika foleni wakisubiri huduma,nilikaa kwenye gogo fulani nikisubiri zamu yangu.Nikiwa pale ghafla nilianza kusikia harufu kali ya marashi.Harufu hiyo ilifanana na ile ya jini Vumina,niligeuka na kuangaza macho huku na kule.Pembeni yangu nikamuona Vumina akiwa katika foleni ya waliosubiri kupata huduma ya Mganga Njugo.
Nilistuka sana hasa baada ya kuona sura ya hasira iliyokuwa imeuvaa uso wa vumina.
Amefikaje hapa ikiwa mwanzo sikumuona?.Nilijiuliza kwa fadhaa.Kwa haraka nikatoka mpaka nje ya ua wa eneo lile nikachukua pikipiki yangu niliyoazima nikaanza safari ya kurudi nyumbani.
Nikiwa njiani ghafla Vumina akatokea mbele yangu.Macho yake yalijaa wekundu kutokana na hasira.Sura yake ilitisha kwa mikunjo ya hasira.Kwa sasa alikuwa amevaa gauni jekundu na kujitandia upande wa kitambaa chekundu.Harufu kali ya marashi ilisambaa eneo zima la chini ya mti wa mbuyu katika barabara hiyo.Nilikamata breki kwa nguvu na kusababisha pikipiki liyumbe kidogo,nikajizatiti na kulisimamisha vizuri.
"Hivi unazani utaweza kuniepuka Lameck,hata uende ulaya hukohuko nitakufuta,labda uingie chini ya ardhi kidogo ndiyo utanipa kazi ya kukupata.
Nakupenda sana Lameck ndiyo maana unaona nimeshindwa kukudhuru ingawa ulitaka kunisaliti.
Nakupa onyo, usijaribu hata sikumoja kuniendea kwa waganga kwani juu ya ardhi hakuna kiumbe yeyote anayeweza kushindana na mimi Vumina mtoto wa mfalme wa majini wa chini ya bahari.
Namalizia kwa kukupa chaguo moja tu.Ukubali kuishi na mimi kama mume na mke,nikupe utajiri mkubwa na niiache hai familia yako au ukatae niue mkeo pamoja na mtoto na unioe kwa lazima,sina mengi ya kusema.Usiku ntakuja kuchukua majibu yako".Alimaliza Vumina na kutoweka.
Ghafla na mimi nilijikuta nje ya nyumba ya alliyeniazima pikipiki.Kwa kweli ilinishangaza kwani ilikuwa ni tukio la kufumba na kushtukiza.Bahati nzuri hakukuwa na yeyote aliyeshuhudia tukio hilo.
Nilkabidhi pikipiki nikapitia kilabu kilichouza pombe za masikini yaani gongo kutokana na kipato changu kidogo.Lengo lilikuwa kupunguza msongo wa mawazo alioniachi jini Vumia.
Usiku nilirudi nyumbani nikiwa nimelewa chakari jamba ambalo lilimshangaza sana mke wangu kwani haikuwa kawaida yangu kufanya hivyo.
"Unanini siku hizi mume wangu?,mbona unaonekana kutingwa na mawazo sana mpaka unafikia hatua ya kunywa pombe"
Siku mjibu chochote mke wangu zaidi ya kumtazama kiasi cha kusababisha nitoe machozi,kila nilipofikiria juu ya mtihani mzito aliokuwa amenipa jini Vumia ambao ulibakiza saa chache kuwasilishwa.
"Usihofu mume wangu,mungu atasaidia utapata kazi,haya ni mapito tu tunapitia"
Aliniambia mke wangu asiyejua kilichoendelea na kunikumbatia hali iliyozidi kunitia machungu.
"Siwezi kumsaliti mke wangu,sipo tayari kuona mke wangu akifa,lazima iwepo njia ya kupambana na huyu shetani..lazima"niliwaza huku nikilia katika kumbato la mke wangu.
Wazo likanijia..Usiku huohuo nilitoka na kwenda kanisani kwa mchungaji.Nikamueleza yote na mtihani niliopewa na msichana huyo wa kijini.
Mchungaji alinipa pole,tukafanya maombi ya pamoja,akanibariki na kunipatia aya ambazo nilitakiwa kuzisoma kabla ya kulala.
Nilirudi nyumbani nikakuta mke wangu akinisubiri,tukala pamoja chakula cha usiku,tukaanza maombi kisha tukasoma zile aya alizonipatia mchungaji.Kutokana na hofu iliyokuwa moyoni mwangu nililala huku nimewakumbatia mke wangu na mwanangu.
Ghafla,nilistuka usiku.Kiza kilitawala,upepo mkali wa baridi ulipuliza.Nikaangaza macho huku na kule bila kuona chochote.Ghafla macho yangu yakafunguliwa mbele yangu nikamuona jini Vumina.Tulikuwa ndani pori kubwa.Harufu kali ya marashi ilitawala.
Jini vumina akataka nimpatie jibu lake.
Je nini kitaendelea. Usikose muendelezo.
INAPATIKANA YOTE KWA BUKU TU.
0629980412- WHATSAPP @simulizi media
